Monday, March 30, 2009

UMOJA WA VIJANA KWA MASLAHI YA NANI?

Tuna hitaji tupate chombo cha kusemea

Ndugu wasomaji wa blog hii ya vijana, kuna jambo moja linanitanza, ningependa tutafakari kwa pamoja.
Jambo lenyewe ni kuhusu kitu kinachoitwa Umoja wa Vijana, Tangu kuzaliwa kwangu mpaka kukua kwangu sijawahi kusikia kuhusu umoja wa vijana. Hapa sizungumzii umoja wa vijana wa CCM, Chadema, NCCR Mageuzi au sijui chama gani huko.

Nazungumzia umoja wa vijana unaowaunganisha Vijana wote nchini bila kujali itikadi zao za kivyama, kidini, kikabila au kikanda.
Nimekuwa nikijiuliza, hivi sisi tunao umoja wa vijana unatuunganisha vijana wote hapa nchini? Umoja ambao tunaweza kuutumia kama jukwaa letu sisi vijana kusemea mambo yetu na kujadili mustakabali wa maisha yetu?.

Naomba munisaidie wadau, hivi hapa nchini tunao umoja wa Vijana wa aina ninayoizungumzia? Na kama upo, makao makuu yake yako wapi na unafanya nini kwa sasa?
Kama umoja wa vijana wa aina hii haupo, basi nadhani wakati sasa umefika kwa vijana kuuwasha moto, Lipigwe la mgambo ili vijana wote nchini tuungane katika kutetea maslahi yetu, tumekandamizwa kiasi cha kutosha, na sasa nadhani wakati umefika kwa sisi vijana kusema basi imetosha, wazee wakae pembeni vijana tushike hatamu za uongozi katika nchi hii.

Labda wadau walioko ughaibuni watusadie, kutuelimisha kuwa huko waliko vijana wenzetu wamewezaje kuunganisha nguvu zao, na kuisaidia jamii katika kujiletea maendeleo? Na wamewezaje kushirikishwa katika maamuzi ya kiserikali pale yanapozungumziwa mambo yanayowahusu?

Tumekuwa tukiambiwa kuwa vijana ni taifa la kesho, hee! Ni kesho gani hiyo isiyofika? mimi naamini kuwa kesho hiyo haipo na haitakuwepo mpaka tuende kaburuni. Huu ni wakati wa vijana kuingia kwa wingi katika siasa ili tujiletee ukombozi.

Kuna maamuzi mengi mazito yanayowahusu vijana hapa nchini ambayo yamepitishwa na wazee wetu bila kutushirikisha na sasa tunaumia, kwa mfano mfumo wetu wa elimu umepogoka, na umekuwa na mizengwe.
Kuna mambo mengi ambayo yanatuhusu na yanahitaji umoja huru wa vijana usiofungamana na chama chochote ili tuweze kuyasema.

Naomba kuwasilisha…..

12 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sema mwanaharakati, hata mimi nilikuwa huko kwenye harakati za vijana nan labda nikukaribishe kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa TYVA pale karimjee ambapo mimi ntaenda kustaafu harakati hizo. umri umepita lakini pagumu kidogo na sas njikita zaidi katika utambuzi na kujitambua, kuelimishana na kushauriana kwa rika zote jap vijana wanakipaumbele.

nimehamua kukua kiroho safari ndefu inayohitaji matumahini ya kutosha.

endeleza mjadala. sisi hili la baraza la vijana tulilijadili mpaka tukaanza kuonekana magaidi na kufukuziwa mbali pale idara ya vijana. mwisho tuligundua watatupatia hiyo baraza ya vijana butu, waweke vijana wao harafu mulie tuuuu

Rama Msangi said...

Nimepita kusalimia dada
hongera kwa kuamua kuhamishia harakati zako katika ukanda huu
maana wengoi wa wanaharakati wanashindwa kujipa majukwaa ambako watasikika na kusaidiwa sanjari na kusaidia wengine ili kuweza kufikia lengo la kuwa na taifa na hata dunia yenye vijana walio na tija

Koero Mkundi said...

Digna naomba ndoto zako zitimie, lakini kama umesoma maoni ya Kamala, kidogo yananikatisha tamaa.


Hebu ngoja kwanza niulize
Hivi umejibiwa kuwa hili baraza lipo au halipo?

Kama halipo basi kazi ipo maan kma kuna mizengwe kamaalivyosema Kamala, basi utajikuta unazeeka na baraza halijapatikana, sasa sijui utabadili uamuzi na kuzai baraza la wazee, maana mwenzangu umri unakwenda. huko kwenye umoja wa vijana wa vyama vya siasa makamanda wao ni wazee, sasa sijuia hawa wataleta mageuzi gani...

Jitahidi mwanamke labda tutafanikiwa tuko nyuma yako.....

Ramadhani Msangi said...

nimerudi tena kutafakari kwa kina sana maoni ya Kamala. Sijui kama amakumbuka kitu kinaitwa Bunge la Vijana/Bunge Kivuli? Naamini kama ni mdau wa TYVA, hadi hivi sasa kuwa anastaafu, anaelewa kitu hiki, na wakati nikiamini pia kuwa atakuja kukizungumzia siku moja, niahidi kuwa siku si nyingi sana zijazo, nitaandika jambo kuhusu Vijana wa Kitanzania na mtazamo wao

Simon said...

hi,
how nice is yoyr blog,
i like it,
would you mind to follow my blog as well?
http://samvande.blogspot.com

ndesanjo macha said...

Umoja wa Vijana (ambao wakati mwingine huongozwa na wazee) ni wa faida ya "wa-twawala" hasa wakati wa uchaguzi!

Anonymous said...

Tanzania na watanzania wanatakiwa kujituma katika kila jambo na ndipo wataweza kufanikiwa maishani. Kama ni ajira na wazisake kwa sana na kuhakikisha wanazifuatilia na kuzipata.

kwa kila jambo wanalolifanya litafanikiwa endapo watakuwa makini na kumaanisha kile ambacho wanakikusudia na kutia bidii sana.

www.ajirazetu.blogspot.com/www.harusiyetu.blogspot.com

jual obat perangsang said...

greetings
obat perangsang | obat kuat | alat bantu sex

Vimax Asli said...

nice blog and article

Meizitang Botanical said...

thanks for sharing

Obat Vimax said...

i like it this blog

poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605