Friday, March 27, 2009

HEBU TUTAFAKARI KWA KINA

Wamepoteza matumaini kabisa

Hivi karibuni nilihudhuria kongamano moja la vijana, ambalo lilikuwa likijadili changamoto zinazowakabili vijana katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na matatizo ya kuyumba kwa uchumi.

Mmojawapo wa waliokuwa wawezeshaji wa kongamano hilo alikuwepo raia mmoja kutoka nchini Marekani. Mwezeshaji huyo alisema kuwa katika kipindi hiki ambacho uchumi umeyumba dunianai waaathirika wakubwa ni vijana, kwani kuna mamilioni ya vijana hapa dunianai wamepoteza ajira na hawajuia hatma yao. Alisema kuwa nchi za ulaya na Marekani anakotoka kuna kundi kubwa la vijana ambao wametupwa nje ya ajira na sasa hivi wana hali mbaya sana kimaisha.

Aliendelea kusema kwamba mfumo wa elimu katika nchi nyingi hauwaandai vijana kujiajiri na badala yake huwaandaa kuajiriwa, na hiyo ndio changamoto wanayopata vijana wengi sana katika kipindi hiki kwa kuwa walisoma wakitegemea zaidi ajira na sasa hivi wanajikuta wakiwa nje ajira na hakuna pa kukimbilia kwani kila mtu amejengwa kiakili kuwa kusoma ni kuajiriwa na ukimwambia ajiajiri unakuwa kama unampa kitendawili kigumu asichoweza kukitegua.

Mwezeshaji huyo alishauri kuwa, kuna haja ya kubadili aina ya ufundishaji mashuleni, pamoja na masomo ya kitaaluma lakini elimu ya ujasiriliamali ipewe kipaumbele zaidi ili kuwawezesha vijana kukabiliana na chanagamoto kama hizi zinapotokea.

Hii naona ni changamoto kwetu sisi vijana, inabidi tuanze kuangalia mustakabali wetu kwa jicho la tatu. Je kuna haja ya kusoma huku tukitegemea ajira au tubadili mtazamo wetu na kuangalaia zaidi namna ya kujiajiri?
Je mfumo wetu wa elimu unakidhi hali halisi tuliyo nayo sasa au ubadilishwe kabisa na kuanzishwa mfumo utakaokidhi matakwa ya hali tuliyo nayo sasa.

Kuna wakati nilisoma mjadala mmoja aliouanzisha dada Koero pale kwenye kibaraza chake cha Vukani, akiuliza “Msomi hasa ni nani?” Sidhani kama swali lile lilijibiwa ipasavyo kwani niliufuatilia sana ule mjadala lakini nikaachwa hewani nisijue niamini nini?
Mitazamo ilikuwa ni mingi na kukinzana kulikuwa kwingi pia, kwa hiyo mwishio wa siku nikaachwa bila jibu.

Naomba tutafakari kwa kina, nini kifanyike ili kukabiliana na changamoto kama hizi za kuyumba kwa uchumi?
Hapa tunatafuta Muarobaini utakaotuvusha hapa tulipo na wakati huo huo tukiweka kinga kwa majanga ya namna hii huko mbeleni

Naomba kuwasilisha

26 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Heshima kwako Dada.
Nimefurahi namna ambavyo umeweza kuelezea tatizo hilo na namna wengine wanavyoliona.
Ni kweli kuwa kama kuna tatizo katika Tanzania, basi mojawapo ni mfumo wa elimu nchini mwetu.
Ungekuwa katika hali ya kumuwezesha mtanzania kuyatumia vema mazingira na rasilimali alizojaaliwa kuwa nazo ingesaidia saaana. Lakini tunakaririshwa mengi tusiyohitaji ama tunayohitaji lakini hayapatikani katika mazingira yetu.
Leo hii mtu anayesoma VETA anakosomea namna ya kutengeneza na kukarabati vitu ambavyo viko ktk mazingira yake anaonekana hana elimu. Wanataka aliyekwenda mbali kuliko uwezo wa mazingira na uwezeshaji wa nchi.
Lakini tukianza na kufunza watu kulingana na mazingira yetu tutaweza kupiga hatua.
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa ni juzi tu nimetoka huko nyumbani nimesikia ya kwamba sasa wanataka kuanzisha kufundisha masomo yote kwa kiingireza yaani sec. Nikawa najiuliza sasa hawa watu kweli wanawaza nini mtu ameanza darasa la kwanza mpaka la saba masomo yote kwa kiswahili isipokuwa kiingereza. Je kweli huyu mwanafunzi hatakosa kupata F F na F amalizapo form four?

Ni afadhali kabisa wangeamua kufundisha kiswahilöi kwani ni lugha tunayoisema kila siku. Kwani hapo kungekuwa na matokeo mazuri sana. Yaani tungepiga hatua kubwaaaa

Bwaya said...

Digna,

Mjadala ule wa Dada Koero haukufikia hitimisho (kama ilivyo mijadala mingi ya blogu) kwa sababu ya uhaba wa wachangiaji. Mijadala kama ile inahitaji mawazo tofauti tofauti kutoka kwa watu tofauti tofauti. Faida ya blogu ni kwamba tunaweza kuiendeleza mijadala wakati wowote wachangiaji wanapoamua kufanya hivyo.

Kuhusu elimu. Ipo haja ya kuvunja vunja kila kitu na kuanza upya.
Mfumo wa elimu yetu usipofumuliwa, mentaliti iliyopo itaendelea kututesa sana na tutatikiswa vibaya. Hivi sasa elimu imekaa mkao wa ofisi ofisi. Mwanafunzi anapoanza kidato cha kwanza anaota ndoto za ajira. Alama nzuri zina maana ya ofisi nzuri mbeleni (iwe serikalini ama kwenye shirika maarufu). Si ufahamu, si maarifa. Ni cheti halafu kazi.

Elimu yetu inatufundisha kukumbuka na sio kuchambua. Elimu yetu hailengi kutufanya tujivunie maarifa. Inalenga tujionee ufahari idadi na madaraja ya vyeti.

Katika hali hii, wahitimu wanaomaliza vyuo wanajikuta wakipigana vikumbo kuajiriwa. Na wakiajiriwa wanadhani imetosha. Na
'wasomi' wajasiriamali wanaonekana 'alosto', watu waliopoteza mwelekeo.

Ni wazi katika hali ya sasa ya uchumi, waswahili tutaathirika sana.

Tufanyeje? Naona tuachane na kutukuza vyeti. Madarasa yawe sehemu ya kujadili mambo yanayohusiana na maisha ya kawaida ya mwanafunzi. Sioni sababu ya kukaririshana nadharia zisizo halisi katika maisha yetu. Kwa maneno machache zaidi namaanisha elimu iwe ni stadi ya matatizo yetu katika specializations zinazogusa maisha ya watu wetu.

Vinginevyo tutatikisika sana.

Bennet said...

Kujiajiri ni kuzuri kwa sababu kuna kupa uhuru wa kufnya mambo yako namna ile unavyo taka, napia kuajiriwa ni kuzuri kwa sababu ya uhakika wa maslahi mwisho wa mwezi yaani mshahara. lakini cha muhimu unapoajiriwa ni kuwa na kipato cha ziada kama biashara, ukulima, ufugaji au hata chochote ambacho kitakuongezea kipato chako

Elimu yetu haitoshelezi kujiajiri katika mazingira yetu ila kama unania ya kujiajiri nina hakika mazingira jumlisha na elimu yako yatakusaidia kuweza kujiajiri

PASSION4FASHION.TZ said...

Digna mpenzi kumbe hiki ndio kibaraza chako! haya leo nimepita kusalimia nitarudi baadae, safi sana blog imetulia hongera sana.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mimi hata nasita kuiita hii elimu tuliyonayo kuwa ni elimu. Siamini kama kukesha usiku ukikariri vitu usivyovielewa vina maana na faida gani kwako na jamii yako kuwa ni elimu. Niligombana sana mwalimu wangu wa Fizikia enzi zile za kuchagua "combination" baada ya kumaliza kidato cha nne. Alitaka nichague PCB kama combination ya kwanza. Nilimkubalia na alipoondoka nikachana fomu na kujaza upya - HGK. Nilitaka kusoma vitabu vya Kiswahili, Historia yetu na Pysical Geography - mambo ambayo angalau ningeweza kushabihiana nayo! Nilikuwa nimechoka kukariri mambo ambayo sikujua yalikuwa na maana gani. Kama alivyosema Bwaya na Mzee wa Changamoto inabidi twende kwenye 'drawing board" na kuanza upya.

Bwaya said...

Masangu, naamini sayansi ni fani yenye mchango muhimu katika maendeleo ya nchi hii. Ni bahati mbaya kwamba, imepuuzwa.

Mimi nilichagua kusoma sayansi. Matarajio yangu ya enzi hizo sijayaona mpaka sasa. Nilichokiona walau kwa sasa ni kwamba kwa namna sayansi inavyofundishwa tunajikuta tukishindwa kuitumia ili kukabiliana na changamoto zetu.

Hatufundishwi sayansi, badala yake tunafunzwa historia yake!

Ni bahati mbaya kwamba kwa mazingira haya tunashindwa kuwa wanasayansi wa kweli, na badala yake tunabaki kuwa watu waliomeza masimulizi ya kisayansi yasiyoweza kutumika katika uwanja wenyewe wa kisayansi ili kuleta mabadiliko yanayotarajiwa.

Kujiajiri kwa hiki kinachoitwa sayansi katika mazingira yetu ni kazi ngumu isipokuwa labda kufungua darasa ili kuwafundisha na wengine hayo hayo ambayo hata wewe hujui uyatumie vipi.

Kissima said...

Hivi aliyesoma ktk mfumo huu wa kwetu wa elimu na yule ambaye hajasoma,au aliyejua kusoma na kuandika tu wanatofauti au hawana,? Ni dhahiri kuwa wanatofauti kubwa tu.Hii ni ishara iliyowazi kuwa pamoja na uduni wa elimu inayotolewa pia inaleta mageuzi makubwa kifikra na kiakili kwa wale walioipitia.
Mimi nadhani mitizamo yetu kuhusu elimu ndio inatakiwa kubadilika.,Erick Shigongo na Nyambari Nyangwine ni baadhi ya watu waliojiajiri na wanaotumia elimu yao vizuri ktk kuleta maendeleo yao na ya wengine,ni mfano mzuri wa kuigwa.Kwa hali ya Tanzania sio siri mtu kujiajiri ni vigumu kulingana na hali ya umasikini lakini mtu anaweza kuajiriwa na baadae akaanzisha miradi yake na kuwapatia wengine ajira.Ni wachache sana wenye uwezo wa kuanzisha miradi yao wenyewe na mara nyingi hutegemea na uwezo wa ndugu au familia.
Mwenye uwezo wa kujiajiri baada ya kumaliza elimu yake ajiajiri ili atoe nafasi kwa wasio na uwezo wa kujiajiri, wale walioajiriwa wakipata uwezo watumie uwezo wao wa elimu yao ktk kucreate miradi ambayo itatoa ajira kwa wengine mbali na wao kufaidika.

Malkiory said...

Kwanza napenda kumpongeza mtoa mada, pili wachangiaje wote kwa mawazo yenu mazuri na ya kujenga.

Nadhani tatizo kubwa la mfumo wa elimu yetu ni mitaala mibovu ambayo tumeirithi kwa wakoloni.

Watanzania bado tuendeleza kasumba ambayo imeshajengeka katika jamii yetu, ya kuwa elimu bora ni ile inayotolewa kwa lungha ya kigeni.

Kinachohitajika kwa sasa ni kwa watanzania ni kubadilika kifikra na kuelewa kuwa muhimu ni ujuzi na maarifa ambayo humfanya mtu kubiliana vema na mazingira yake bila kujali huo ujuzi na maarifa zilipatikana kwa lugha gani.

Kama walivyochangia wadau wengine, binafsi ninakerwa sana na suala hili la utoaji wa elimu ya msingi kwa lugha ya kiswahili na baada ya hapo kila kitu kinageuka na kuwa kiingereza, hali hii inaleta elemavu katika ubora wa elimu yetu.

Katika kukabiliana na suala la kujiari bado suala la elimu ya ufundi(polytechnics, professional schools) lazima litiliwe mkazo.

EVARIST said...

Moja ya mambo yaliyomsukuma Baba wa Taifa kuja na sera ya Elimu ni Kujitegemea ni mtizamo wake kwamba elimu baada ya uhuru ilikuwa ni ya kumwandaa mwanafunzi kuajiriwa (as opposed to kujiajiri) na kimsingi ilikuwa na mtizamo wa kimagharibi zaidi (neno jepesi la kibepari) kuliko wa kijamii yetu.

Pengine ni muhimu kujiuliza kwanini Elimu ni Kujitegemea (Education for Self-Reliance) haikufanikiwa.Maana mengi ya haya tunayoyatamani sasa yalikuwa sehemu muhimu za sera hiyo.

Nyerere alitamani wanafunzi wengi wapate elimu ya msingi darasani na kisha wakaitumie vijijini,huku wengine wakijiendeleza kwenye fani za ufundi kwa minajili ileile ya kuitumikia jamii,na wachache waendelee hatua ya sekondari na hatimaye chuo kikuu,wote kwa mtazamo uleule wa kuitumikia jamii.Lengo halikuwa kudumaza elimu bali kuiweka jamii mbele as opposed to mtu binafsi.Na eneo la msisitizo zaidi lilikuwa KILIMO ambacho kilikuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wetu.

Anyway,pengine tuiweke kando historia angalau kwa muda huu.Wazo la kujiajiri ni muhimu lakini mazingira tuliyonayo yanakwamisha kila kitu.WAnaojaribu kujiajiri kwenye kilimo "wanafisadiwa" na vyama vya ushirika.Mabenki yanayotarajiwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali yanawaogopa "wajasiriamali halisi" kama ukoma:kisingizio eti wako risky au hawakopesheki,lakini tatizo kubwa zaidi ni pale wenye uwezo (neno jepesi la vigogo,mafisadi,etc) wanapojivika ulalahoi na kudowea mipango endelevu iliyoasisiwa kuwakwamua wajasiriamali.Mwenye muda afanye assessment ya "Mabilioni ya JK"! kuelewa nachokipigia mstari hapa.

Hivi Wamachinga si ni sehemu ya waliojiajiri?Lakini sijui ni wangapi kati yao wenye hamu ya kuendelea kuwa self-employed as Wamachinga kwa namna Mamlaka zinavyowapelekesha mithili ya wezi au "outcasts" flani katika jamii.

Okay,tubali mfumo wetu wa elimu ili ulenge zaidi kwenye kujiajiri badala ya kuajiriwa.Swali:wajiajiri wapi kwenye nafuu?Kwenye kilimo ndio hivyo,kwenye ufungaji ndiko wengine wanajikuta kwenye migogoro kama ya huko Kilosa ambako vigogo wanataka "nafasi ya kutosha kwenye sekta hiyo"...mifano ni mingi.

Pengine wakati tunaangalia ajira kwa wahitimu tuwe specific tunawazungumzia watu wa aina gani.Maana kama baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu wanashindwa kutumia elimu na ujuzi wao kujiariji sijui tutegemee nini kwa wahitimu wa shule ya msingi na sekondari.

Pengine jingine lililo muhimu ni hili suala la utandawazi ambalo linaifanya dunia kuwa mithili ya kijiji.Sasa sie tunaweza kung'ang'ania tucheze mchezo huu kwa sheria tunazotaka sie lakini kwa bahati mbaya mfumo dhalimu uliopo hautupi nafasi hiyo.Ni muhimu kuenzi lugha yetu ya taifa,kwa mfano,lakini katika mfumo MUFILISI ambao anayemuda Kiingereza,Kifaransa na lugha nyingine za "kimataifa" ndiye anaonekana mwenye sifa,matokeo yake ndio hayo ya Wakenya (kwa mfano) kuchukua ajira zetu (kwa madai wanamudu zaidi kimombo kuliko sie) ilhali sie tunaishia kupeleka watoto kwenye "international schools" za Kenya na Uganda kusaka elimu bora.Yaani wenzetu wanaleta wafanyakazi sie tunapeleka wanafunzi!

Ni muhimu kuzingatia kuwa tunaishi kwenye mfumo dhalimu,mfumo wa kibaguzi wa "survival of the fittest of the fittest" na ni nadra kwa akina sie tunaotegemea fadhila za watengeneza sera za dunia kuwa na fursa ya kujiamulia baadhi ya mambo yetu muhimu.

Binafsi najitahidi sana kuepuka generalisation kuhusu Watanzania,taifa lenye takriban watu milioni 40 na makabila zaidi ya 120.Hivi "Watanzania wenye mentality kuwa elimu inayotolewa kwa lugha ya kigeni ni bora zaidi" ni wapi hao?Watu wa Kilimanjaro na Kagera (kwa mifano) waliobahatika kutangulia kielimu kwa sababu mbalimbali (ukoloni,wamisionari,mandhari,nk),baadhi ya makabila ya pwani yaliweka msisitizo zaidi kwenye elimu ya kiroho secular education,au katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya kusini ambako mchanganyiko wa siasa,hali ya hewa na tamaduni ni kikwazo?

Tunapowahukumu Watanzania kuwa na fikra za za aina hiyo kwanini tunasahau mifano rahisi tu ya sie tunaoblogu?Mbona wengi wetu tunaendeleza shughuli hii kwa lugha yetu maridhawa kiasi cha baadhi ya wenzetu wa Afrika Mashariki kuleta husda na kudai Watanzania wengi wana-blog kwa Kiswahili kwa vile Kiingereza ni mgogoro!?

Japo,kama alivyoeleza dada Digna kuwa waathirika wakubwa wa msukosuko wa sasa wa uchumi wa dunia ni vijana,binafsi nayajumuisha na makundi "yaliyozoeleka" ikiwa ni pamoja na walemavu,watoto,akinamama (hususan wa vijijini) na wazee.Katika jamii zetu ambazo mfumo dume unamfanya baba/mume kuwa "mwangalizi wa familia" ni dhahiri basi pindi akipunguzwa kazi,akikosa soko la mazao,nk kutokana na msukosuko huu wa uchumi inamaanisha mama/mke na watoto nao wataathirika.Watoto kwa upekee wao hawana msemaji na hawana uwakilishi katika maamuzi mengi yanayohusu hatma zao (tunapoongelea elimu ni muhimu pia kukumbuka nafasi ya wazazi katika chaguzi za maisha zinazofanywa na watoto wao).Walemavu na wazee ni "watengwa" wa muda mrefu katika nchi zetu masikini ambazo hazina uwezo wa kuhudumia makundi ya flani (mengi) ya jamii.

Tufanyeje?La haraka na lililo ndani ya uwezo wetu ni kuwakalia kooni wadaiwa (neno pole la majambazi) wetu kama mafisadi wa Richmond,Kagoda,nk...na pia kuangalia upya vipaumbele vyetu.Kwa mtaji huu wa mshahara wa Mbunge Milioni 7 kwa wabunge zaidi ya 200,mashangingi mapya takriban kila mwaka (na hivi tuna wakuu wapya wa wilaya si ajabu wakataka mapya pia),na matumizi mengine ya "kitajiri" ni dhahiri tutaumia pindi wafadhili wetu (ambao nao "wanapigika vilivyo") watapopunguza au kukata misaada.

EVARIST said...

Kuna kitabu kimoja, "The Making of a Periphery: Economic development and cultural enecounters in Southern Tanzania" (Kimehaririwa na Pekka Seppala na Bertha Koda,1998) nadhani kinatoa picha mwanana kuhusiana na mada hii.Kuna chapter ya Luanda na Luhanjo "The south-east economic backwater and the urban floating Machinga" inatoa mwanga mzuri pia kuhusiana na dhahma wanazokumbana nazo vijana vijijini na hatimaye kukimbilia mijini.

Koero Mkundi said...

Digna, ule mjadala wa msomi hasa ni nani sijui hata uliishaje?
Lakini naona hata wewe unayo nafasi ya kuuendeleza, kwani tunaweza kuugeuza huu mjadala na kuwa kama mbio za vijiti mapaka kitaeleweka

Shimba ya buhongo said...

Kwanza hodiii! Kisha kwa sababu mtachelewa kunijibu najikaribisha mwenyewe. Karibu nani wewe? pita mlango umerudishiwa tu.Asante.
Hili suala la elimu wa ndugu mnajaribu kulirahisha mno. Kufundisha kwa kiswahili si sababu ya kuwafanya wanafunzi waelewe vizuri. Maana kama ingekuwa ndivyo basi somo la kiswahili watu wangekuwa wanajenga vibanda tu 'A' kwenye somo la kiswahili. Lakini wapi wanafeli kuliko hata kiingereza. Kwa saili hii mwisho tutasema kwa wanafunzi wa vijjini tutumie lugha za makabila. Halafu tukisema eti tutumie kiswahili hivyo vitabu vyenyewe vipo? Na tena dunia ya leo ni ya saa ya nzi na teke linalokuijia hicho kiswahili mwanafunzi asiyejua lugha zinazotumika huko atapataje maarifa yaliyoko kwenye mtandao?
NIsije kuandika gazeti zima, nakataa katakata kudai elimu yetu ni mbovu kiasi hicho. Tunao madaktari waliobobea (taaluma ambayo ndugu Matondo aliikimbia) hawa wote wamesoma kwa elimu hii hii tunayoiponda hapa. Elimu kama elimu siyo mbaya bali mazingira ya utoaji wa elimu ndio mabaya. Mwalimu asiyethaminika hawezi kuwa na morali wa kufundisha. Mwalimu ambaye yeye mwenye amefeli atafundisha kitu gani? Mwanafunzi asiyepewa homework ataelewaje? Mwanafunzi anayefunga daftari (maana hawana vitabu)mwalimu anapoondoka na haligusi tena mpaka siku ya kipindi kingine hata ukimfundisha kwa lugha gani hawezi kuwa naufahamu. Mwanafunzi anayeenda shule wakati hajatia kitu tumboni isipokuwa (msimu wa maembe)kweli ataweza kusikiliza darasani? Hata hizo zinazoitwa shule za kata, watu wanaweka majengohalafu wanaita shule kidato cha kwanza mpaka cha nne walimu watano! Jamani tuwe wakweli shule ya namna hii hata ukibadilisha lugha na mfumo wa elimu kweli itakuwa na maendeleo yeyote? Ni mengi mno yanayoathiri elimu yetu kabla hatukomalia lugha

Anonymous said...

Tanzania na watanzania wanatakiwa kujituma katika kila jambo na ndipo wataweza kufanikiwa maishani. Kama ni ajira na wazisake kwa sana na kuhakikisha wanazifuatilia na kuzipata.

kwa kila jambo wanalolifanya litafanikiwa endapo watakuwa makini na kumaanisha kile ambacho wanakikusudia na kutia bidii sana.

www.ajirazetu.blogspot.com/www.harusiyetu.blogspot.com

Crystal X said...

salamu kutoka kwa rafiki yako katika Indonesia

toko buku islam said...

thank you

Obat Vimax said...

nice blog and article

Obat Perangsang Wanita said...

i like this blog

Meizitang Botanical said...

thanks for sharing

Vimax Canada said...

thanks for sharing, goods article

Selaput Dara Buatan said...

Nice article and good information

poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605

poker uang asli said...jasa seo
jasa seo indonesia
jasa seo terpercaya
seo indonesia
jasa seo web judi
jasa buat website
jasa pembuatan website

Sbobet
Agen Sbobet
Agen IBcbet
agen MAXBET
bandar bola
judi bola
judi online
taruhan bola
agen resmi sbobet
agen bola
agen bola terpercaya
agen sbobet terpercaya

agen poker
poker online
agen poker terbaik
agen poker terpercaya
poker uang asli
situs poker

agen poker
poker online
agen poker terbaik
agen poker terpercaya
poker uang asli

agen ibcbet terpercaya said...


agen poker
poker online
pagen poker terbaik
agen poker terpercaya
poker uang asli

sabung ayam
adu ayam
ngadu ayam
laga ayam
permainan adu ayam
ayam petarung
ayam sabung
ngadu ayam jago
adu ayam online
taruhan ayam
sabung ayam terbaik
judi online ayam
ayam sabung online
judi adu ayam
situs sabung online
judi sabung online
permainan laga ayam
sabung online
sbobet
agen sbo
agen sbobet
agen sbobet terbaik
agen sbobet terpercaya
sbobet asia
ibcbet
agen ibcbet
agen ibcbet terbaik
agen ibcbet terpercaya
ibcbet online
sbobet online

poker online asli said...agen casino indonesia
agen judi sbobet
agen sbobet indonesia
agen sbo
agen sbobet terpercaya
agen sbobet
agen sbo terpercaya
agen judi terpercaya
sbosports
agent sbobet
agen sbobet indonesia
bandar judi terpercaya
agen judi bola terpercaya
agen judi ibcbet
sbobet indonesia
agen bola online
bandar judi bola
master agen betting online
bandar bola sbobet terpercaya
judi online

BANDARQ
Agen Poker
situs poker
poker online
Judi Poker Online
situs poker online terpercaya
Poker Online Terpercaya
poker uang asli
Domino QQ
Domino Poker
Capsa Online
QQ Online
Ceme Online
Blackjack Online
Poker Online Indonesia
Agen poker online
poker online asli
agen poker terbaik
agen poker terpercaya
situs poker uang asli

BANDARQ
Agen Poker
situs poker
poker online
Judi Poker Online
situs poker online terpercaya
Poker Online Terpercaya
poker uang asli
Domino QQ
Domino Poker
Capsa Online
QQ Online
Ceme Online
Blackjack Online
Poker Online Indonesia
Agen poker online
poker online asli
agen poker terbaik
agen poker terpercaya
situs poker uang asli

gen resmi piala dunia 2018 said...


agen bola terpercaya
pasang bola
judi bola online
agen bola terpercaya

Agen bola
Judi Online
Agen Bola Online

casino online terbaik
casino online
judi online
agen casino online
judi live casino

agen sbobet terpercaya
agen bola,
judi bola,
BANDAR bola ONLINE terpercaya
BANDAR bola ONLINE terpercaya
agen sbobet terpercaya
judi online,
agen judi, bola online

agen judi
agen bola
situs judi
judi bola
judi online
bandar bola
bandar judi
situs taruhan
taruhan bola
taruhan online
situs judi bola
situs judi online
situs judi terpercaya
agen bola terpercaya
agen judi online
judi online terpercaya
agen judi terpercaya
bandar judi online
bandar bola terpercaya
judi bola online
agen piala dunia 2018
bandar piala dunia 2018
situs taruhan piala dunia 2018
situs judi piala dunia 2018
agen resmi piala dunia 2018