Friday, April 17, 2009

2010 NAHISI WATU WATAKIMBIA TAALUMA ZAO!

Ushindani utakuwa mkubwa

Ndugu wasomaji wa blog hii, kwanza samahani kwa kutoonekana katika kibaraza hiki kwa muda mrefu kidogo. Hii nikutokana na mlundikano wa majukumu niliojiwekea, ambayo naoan kama vile yananielemea. Hata hivyo kwa kuwa maji nimeshayavulia nguo sina budi kuyaoga.

Ndugu wasomaji na wanablog wenzangu ukimya wangu haukuwa ni wa bure, bali pamoja na mambo mengine, lakini nilikuwa najaribu kutafuta changamoto mbalimbali zinazotukabili sisi vijana, ili niweze kuziweka hapa tuweze kujadili kwa pamoja.

Kwa kuanzia, kuna jambo moja ambalo nimekuwa nikijiuliza, naamini labda si mimi peke yangu, lakini inawezekana wapo ambao nao kwa upande wao wanajiuliza kuhusu jambo hili.

Kama inavyojulikana kuwa Mwaka 2010 ni mwaka wa uchaguzi mkuu, uchaguzi ambao utatupa fursa sisi wananchi kumchagua Rais wa nchi hii pamoja na Wabunge,
Swali ninalojiuliza ni hili, kwa kuwa imeonekana kuwa siasa ina tija kuliko kazi nyingine za kitaaluma, kazi kama Uhadhiri, Udaktari, uinjinia uhasibu, uanasheria nakadhalika nakadhalika.
Hii haiashirii kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wasomi wetu, hasa vijana kukimbilia siasa kwa wingi na kutelekeza taaluma zao ili kujihakikishia kipato?

Kama inavyojulikana kuwa mishahara ya serikali ni midogo na hivyo kusababisha pensheni nayo kuwa kiduchu, sasa huu si ushahidi tosha kuwa kazi za kitaaluma hazilipi, na badala yake siasa ndio yenye kulipa?

Wote tumemsikia Mheshimiwa Wilbrod Slaa mbunge wa Karatu kupitia CHADEMA, akielezea kuhusu ukwasi unaopatikana pale Bungeni.

Je hii haiashirii kwamba huenda mwakani nchi ikakumbwa na uhaba mkubwa wa wataalamu hawa katika sekta za Elimu, afya, Miundombinu, Sheria, na nyingenezo?

Mimi sio mtabiri, lakini kila nikiangalia kwa makini, naona kama hili huenda likatufika.
Hii nadhani ni changamoto yetu wote kama anavyosema Mzee wa Changamoto kaka Mubelwa Bandio.

13 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Amani na Upendo kwako Da Digna.
Tatizo la nyumbani si mafao tu, bali HESHIMA NA THAMANI ya kazi zenye maana inapungua na kutoweka. Angalia kazi kama ualimu ambayo ingestahili kuwa na heshima kubwa kutokana na matokeo ya kazi hiyo, inadharaulika na kutothaminiwa na serikali kiasi kwamba walimu ni kati ya watu wa mwisho kutekelezewa mahitaji yao. Tazama WAUGUZI. Nao japo hali yao si kama walimu, lakini wanakuwa na hadhi na vitendea kazi duni mpaka unawaonea huruma. Vikosi vya zimamoto. Ni muhimu kwetu na wawekezaji aa wajasiriamali wanaotaka kuwekeza nyumbani na ukizingatia hitilafu za umeme zinazosababisha moto mara kwa mara. Vitendea kazi vyao ni zaidi ya lawama kwao. Angalia miundo mbinu kama maji taka mijini (na hasa Dar). Haithaminiki na hakuna mwenye mpango nayo. Sasa sijui ukisomea kazi hiyo utathaminika vipi wakati usomeacho hakithaminiki. Ndio maana hakuna anayesumbuka kuboresha mifumo ya maji taka licha ja jiji kufurika kila inyeshapo mvua ya nusu saa.
Lakini wanasiasa? Nahdnai mishahara yao huwa ni "advance". Yaani wanalipwa hata kabla hawajaenda kusinzia bungeni. Namkumbuka mtu mmoja aliyesema ulimwenguni huwezi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja. Lazima ufanye kulingana na umuhimu (priorities) na akasema njia sahihi na rahisi ni ku-"do first things first"
Amani kwako na Ijumaa njema

Albert Kissima said...

Mzee wa changamoto umeongea ukweli mtupu.

Serikali ingekuwa inazijali sekta zote ipasavyo, mimi nadhani kila mmoja angebakia kwenye kazi inayoendana na taaluma yake.

Kweli siasa ina maslahi mazuri lakini pia ni kati ya nyanja ambazo zinahatarisha maisha kupita kiasi.

Katiba ya jamuhuri ya Muungano inasema , mgombea uraisi lazima awe na elimu isiyopungua shahada moja na bila kujali ni elimu gani(kama siko sahihi nisahihisheni) iwe shahada ya ualimu, udactari wa binadamu, usanifu wa majengo, sheria, siasa n.k, sijui kwa nafasi nyingine za uongozi serekalini., hili mwalionaje? Halichangii kwa wasomi kuikimbilia siasa!

Pia yawezekana si wote wanaohitimu kwenye mambo ya siasa wanaingia kwenye siasa, je mtu hawezi kulazimika kuamini kuwa kuna wasomi wanaoenda kwenye siasa kwa sababu ya vipaji ? bila kusahau pia wapo wanaoingia kwenye siasa kwa tamaa tu na si sifa yoyote ya uongozi waliyonayo na pengine hawa ndio wale mafisadi, wala rushwa, wasio na uzalendo hata kidogo?


Kwa upande mwingine jamii pia inahusika kwa kiasi fulani ktk kuwafanya wasomi kuzikimbia fani zao. Jamii huwa inamchukulia msomi kama mtu asiyeshindwa jambo. Utasikia watu wakimwambia mtu aliyekwenda vidato " elimu yako bwana inatosha kabisa kukupa nafasi ya ubunge, hebu changamkia hiyo nafasi" wengine, "hivi huyo anayenadi sera zake anaelimu gani? asijekutuaibisha". Wengine wanamfuata msomi mwalimu na kumwambia kutokana na umaarufu wake kama mwalimu akigombea ubunge,udiwani n.k hatakosa, na kweli mtu anafanikiwa na kisha kuachana kabisa na ualimu au taaluma yake na kujikita kwenye siasa.

Evarist Chahali said...

Dada yangu Digna,kwa Tanzania ya sasa siasa imegeuka ajira,lakini ajira isiyoangalia sifa za candidate (iwe ni taaluma au uwezo wa kuongoza).The key word is MONEY,na sio fedha ndogo bali mamilioni ya shilingi.Daktari,injinia au mwanataaluma atakaejaribu kukimbilia huko sharti awe na "pochi la nguvu" ili aweze kufanikiwa kupata angalau udiwani.

Kwa mtizamo wangu,nadhani wanataaluma tunaoweza kuwakosa baada ya 2010 ni wale tu wenye uwezo mkubwa wa kifedha wa kuwawezesha kugombea nafasi za kisiasa.

Na ni kwa sababu hii ya kuhitaji uwekezaji mkubwa wa fedha kwa minajili ya kupata nafasi za uongozi ndio tunaishia kupata viongozi wanaohangaikia zaidi maslahi yao kuliko ya wananchi wa kawaida.Na pengine hatuwezi kuwalaumu kwani picha inayojengeka ni kuwa wamenunua uongozi huo,na ukishanunua kitu kinakuwa chako!Sort of...

Waheshimiwa pia wanakuwa bize zaidi wakati wa uongozi wao kuhakikisha wanarejesha gharama walizotumia kununua nafasi zao.Nakumbuka stori moja ya Mbunge wa zamani wa jimbo moja la uchaguzi jijini Dar inayoeleza kwamba alipofuatwa na wapiga kura wake kumtaka ashughulike masuala flani aliishia kuwatimua kwa kuwaambia:KWANI MLINIPIGIA KURA KWA KUNIPENDA,AU NI ZILE FEDHA NILIZOWAPA WAKATI WA KAMPENI?

Mwisho,sidhani kama kuna ubaya kwa wanataaluma kuingia kwenye siasa IWAPO WATAINGIA HUKO KUTUMIKIA WATANZANIA WENZAO NA SIO WAO BINAFSI.Sioni tatizo tukiwa na wahadhiri watakaoingia bungeni kupigania mazingira mazuri ya elimu,au madaktari watakaoingia bungeni kupigani uboreshaji wa sekta ya afya,au wahasibu watakaopigania kuzingatiwa misingi ya uhasibu (badala ya undugu,ushkaji,rushwa,nk) katika usimamizi wa fedha za umma.

Kwa bahati mbaya,hadi sasa wanataaluma wengi walioamua kubwaga manyanga kwenye fani zao na kuingia kwenye siasa wameshindwa kuwa na manufaa kwa taaluma hizo au taifa kwa ujumla.Na tatizo la msingi ni hilo nililobainisha hapo juu: walitumia fedha nyingi kuingia kwenye siasa,baada ya kupata nafasi hizo za kisiasa wanakuwa bize zaidi ktk kulipa madeni ya "wafadhili" wao kuliko kutumikia taaluma zao na wananchi kwa ujumla.

Safari bado ni ndefu.

MARKUS MPANGALA said...

nakusalimu toka nyasaaa KARIBU SANA NYASA.
nakubaliana na wanazuoni hawa kuwa siasa imekuwa ajira ambayo watu wanaanglia mafao tu bila kujali mafao hayao yanapatikana namna gani, wao wanachojali ni kwamba wamepata kiasi gani na muda gani bila kujali ni uharibu kiasi gani wameuleta katika kusaka mafao yao.
naona wamesema mengi wakubwa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aisee. maisha ya mwili. ni matamu kumbe yana mwisho

Simon Kitururu said...

Digna Upo? Naona kimya mwanakwetu!

Yasinta Ngonyani said...

Yeah! Digna upo wapi maana kimya kimezidi tunakumiss.

Anonymous said...

Hilo ni kweli jwa kias fulani 2. Hilo lingewezekana tu kama kungekuwa na nafas ya mgombea binafsi, lakini kwa kuwa nafasi zenyewe ni za kupeana na kujuana na kwa vile unatakiwa kuwa na pesa za kuhonga then mtumish wa serikali hataweza labda awe fisadi.

Halil Mnzava said...

Leo nimepita hapa.Safi sana

Digna Abrahamu said...

nimerudiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mama

Vimax Pills said...

nice blog

Vimax Asli said...

i like it this information

poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605