Behavefree ni blog itakayokuwa inajadili tabia mbali mbali za vijana ikiwa ni moja ya changamoto zinazowakabili vijana katika kufikia malengo yao ya baadaye katika jamii. Kutokana na changamoto hizo wamewezaje kubadili tabia zao na kufikia malengo yao na hatimaye kupata mafanikio katika kuendesha maisha yao. Pia kutakuwa na habari za kuchangamsha, kufurahisha na kuelimisha.
Friday, November 1, 2013
KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUNA TIJA KWENYE KUBADILI MAISHA
Habari za siku nyingi wasomaji wa kurasa hii, Ni kipindi kirefu sikuitendea haki blog hii,ila namshukuru Mungu kwa sababu nimepata kibali tena nije kushirikishana mawazo chanya ili kubadili mifumo yetu kimaisha ,kisiasa na kiuchumi..
Nimekaa nikatafakari kwa muda mrefu bila majibu lakini kwa sababu tupo hapa kujuzana basi vyema mnisaidie kupambanua na ikiwezekana kupata jibu kama kasi ya mitandao ya kijamii duniani inatija kifursa kwa kijana wa leo na hasa kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania;
Maswali yangu ni haya;
Je, kuna fursa?
Kama zipo ni zipi kwa nafasi yako?
Na je unazitumia kwa ajili ya maendelea yako na kubadilisha mtazamo wako au kwa ajili ya kujifurahisha wewe kama wewe?
Je unakubali kwamba mitandao ya kijamii ni mbadala wa simu katika mawasiliano,masoko, bank na mengine mengi tu!
Hebu tupanue mawazo yetu ili tuweze kunufaika nayo na si bora kuchat,...mpo wapi watu wa computer science hapa hii ni fursa kwenu kutengeneza software zitakazotatua changamoto zinazokabili nchi yetu na za jirani zetu kwa ujumla.........Karibuni sana mchangie.......tusilie ajira hamna wakati zipo.
Subscribe to:
Posts (Atom)